Sunday, 30 November 2014

Uwiiiiiii soma KIMYA KIMYA

Salaam zako Mama Anna Makinda, naomba usome alama za nyakati maisha yanakwenda kasi sana, jana nilikuwa kwenye kikao kilichotafuna muda wangu wote wa siku nzima, lakini nilipigwa simu milango ya saa moja hivi za usiku nikaulizwa, "kaka uko wapi?", "Nipo Moshi Kilimanjaro" nikajibu.
"Umeme upo huko" nikaulizwa tena, nikawaambia "umekatika hivi punde".
Aliyenipigia simu akaniambia kuwa hata Dar es salaam umeme umekatika na amepata taarifa pia kuwa hata Mwanza umeme haukuwepo m...uda huo!!
Nisikuchanganye na hizi habari za umeme, ninachotaka kukwambia huyu aliyenipigia simu ni mdogo wangu wa mwisho sijawahi hata siku moja kumuona akiangalia wala kufuatilia bunge!! Sasa ameanza kufuatilia bunge, najua si yeye pekee wapo wengi sana hawa, kwani jana niliwaona wakifuatilia TV kama vile wanaangalia mechi ya mtani jembe !!
Marehemu baba yangu aliniambia wanawake wembamba woote ni wasumbufu (samahani rafiki zangu wa kike ambao ni wembamba) hata mke wangu alipokuwa mwembamba alikuwa msumbufu sana sasa amenenepa napumua, Mama wa jengoni hebu jitahidi na wewe unenepe, ni heri kero za mke wangu zilikuwa ni kwangu tu, kero zako ni kwa Watanzania wote, usikubali mungu akunyime sura na roho pia!!!

chanzo:
Mkubwa Kambi



KANGI LUGOLA ALIVYOOMBA KUVAA KININJA ILI ACHANGIE RIPOTI YA TEGETA ESCROW BUNGENI

No comments:

Post a Comment