Sunday, 11 January 2015

Hadithi-MWANASHERIA KATILI SEHEMU YA 10

Ilipoishia sehemu ya 9
“Niger action!”Black Chata alimwamuru mwenzake anayeitwa Niger.Mara Niger akatoa bunduki yake na kuwashuti wale askari.Walianguka chini na damu zikatapakaa kila mahali.
Wauguzi walitetemeka sana baada ya kuona askari wameuawa.Mr.Cheo kwa muda huo alikuwa amelala fofofo!wala hajui kinachoendelea.
Sasa endelea........
“Tom fasta!”Black Chata alimshtua kijana mwingine.Tom alitoa mkasi na kwenda moja kwa moja hadi alipolala Mr.Cheo. “Njoo mpanue mdomo”Tom alimwita mwenzake.Yule jamaa alimpanua Mr.Cheo mdomo,mara akashtuka.Alijaribu kuinuka lakini alibanwa kisawasawa.
Alipanuliwa mdomo na kuuvuta ulimi wake nje.Tom alianza kuukata ulimi kwa mkasi.Wale wauguzi wakashindwa kuvumilia mara wakaanza kupiga kelele.Black Chata na wenzake waliwashambulia kwa risasi na kuwaua wote.Maiti zilitapakaa kila upande mle chumbani.Walimaliza kumkata Mr.Cheo ulimi na kumwacha akilia kwa maumivu makali.Niger alimsogelea na kumwambia.. “Ulimi umekuponza”kisha wakaondoka haraka eneo lile.
Walipofika chini waliwasha gari na kutaka kutoka lakini mlinzi aligoma kufungua geti.Aliwafuata na kuwauliza kama wameruhusiwa kuondoka.Walishusha kioo cha gari taratibu na kutoa mdomo wa bunduki na kumwelekezea yule mlinzi.
“Fungua geti kabla hatujakumaliza”mlinzi alifungua geti na gari likaanza kutoka.Kabla hawajafika nje Niger alimshuti yule mlinzi risasi akaanguka chini kisha wakaondoka kwa mwendo wa kasi.
Usiku wa saa saba Nesi mwingine wa zamu alikwenda kumpa dawa Mr.Cheo. “Mungu wangu!!!!mamaaaa!!!”Nesi alipiga kelele baada ya kuona maiti nyingi mle chumbani.Alitoka mbio hadi kwa madaktari na kuwaeleza kila kitu alichokiona.Wote walienda moja kwa moja mpaka mle chumbani.Walishangaa mno walipoziona maiti zaidi ya tano.
Mara moja wakapiga simu kituo cha kati cha polisi kuwataarifu tukio hilo.Machozi yaliwabubujika kama maji walipowaona wauguzi pamoja na maaskari wameuawa. Wakiwa katika hali ya huzuni mara wakasikia sauti ya mguno ikitokea mle mle chumbani. “Mmmh!mmh!!”Walitafuta kila upande mpaka wakampata aliyekuwa anaguna.
“Mr.Cheo pole sana,ndio nilikuwa nakuja kukupa dawa.Hebu tuambie nini kimetokea humu ndani?”Nesi alimpa pole Mr.Cheo na kumtupia swali lakini hakupata jibu lolote.
Mr.Cheo alijaribu kufungua mdomo ili ajibu,damu nyingi zlilimtoka mdomoni na kumfanya ashindwe kuongea.
“Mungu wangu!njooni jamani mnisaidie!!”Nesi aliwaita madaktari kwenda kumwangalia Mr.Cheo.Walimchukua mpaka chumba cha mahututi.Polisi walifika pale hispitalini na getini walikutana na maiti moja ya mlinzi.Walijihami kwa bunduki zao na makoti ya bullet proof.
Waliingia ndani wakapelekwa moja kwa moja hadi kile chumba yalipofanyika mauaji.Walifanya uchunguzi wa risasi zilizotumika kisha wakaruhusu maiti zote sita kupelekwa mochwari baada ya kupiga picha.Madaktari waliokuwa wanamshughulikia Mr.Cheo waligundua kuwa kakatwa ulimi na kipande hakikuonekana.
“Inasikitisha sana hatoweza kuongea tena!”Wale madaktari waliambiana kwa huzuni mno huku wakiendelea na matibabu.
Kesho yake asubuhi wakazi wa jiji la Dar-es-salaam na Tanzania kwa ujumla walikuwa katika simanzi nzito mara baada ya vyombo vya habari kuripoti juu ya tukio la mauaji ya watu sita hospitali ya Muhimbili na mgonjwa mmoja kukatwa ulimi.Walitajwa kwa majina watu waliyouawa ikiwa ni pamoja na polisi wawili waliokuwa wakimlinda Mr.Cheo aliyekatwa ulimi,wauguzi watatu na Nesi mmoja.
“Mamaa!Mungu nisaidie mimi!!mume wangu!! Jamani kawa bubu!!”Mke wa Mr.Cheo alilia kwa uchungu sana alipokuwa anasoma gazeti moja lilliloripoti taarifa hiyo.Alikimbia mpaka nyumbani,alipofika mlangoni akaanguka “Puuuh!!!!”na kupoteza fahamu.Mike alisikia kishindo na kutoka nje ili ajue ni kitu gani hicho kilichoanguka?
“Aunt nini tena!?amka!!”Mike alimwita Aunt yake mara baada ya kufungua mlango na kumwona akiwa amelala chini.
Alijaribu kumnyanyua akashindwa,alikimbia mbio hadi kwa jirani kumwita kijana mmoja.Walisaidiana kumbeba Aunt yake mpaka ndani na kumlaza juu ya kochi na kuanza kumpepea.Machozi yalimdondoka Mike na kumhurumia sana Aunt yake kutokana na hali aliyokuwa nayo.Dakika 15 zilipita ndipo Aunt akaanza kufungua macho.
“Mike!Mike!!Uncle wako Mike!!”Aunt alimwita Mike kwa uchungu na kwa sauti ya chini huku machozi yakimtoka..Mike alishtuka sana.
“Nini tena Aunt!Uncle kafanyaje?”
“Mike inauma sana”
“Niambie Aunt amefariki au?pleas niambie ukweli usinifiche?”Mike alimbembeleza Aunt yake huku naye akilia.
“Mike Uncle wako kakatwa ulimi,sasa hivi ni bubu hawezi tena kuongea.Jamani mimi mbona mikosi hivi?”
Mike alitoa macho kama mjusi aliyebanwa na mlango.Hakuamini alichokisikia,alilia sana tena kwa kwikwi “Mungu tusaidie sisi kwanini kila balaa kwetu tu jamani!?”
Mke wa Uncle alizungumza maneno ya uchungu mno.Nusu saa ilipita,Aunt aliamua kujiandaa kwenda hospitalini kumwangalia mumewe.Waliondoka pamoja na Mike mpaka Muhimbili.
Siku hiyo kulikuwa na ulinzi mkubwa sana.Askari polisi walitanda kila kona ya hospitali hiyo kutokana na tukio lilitokea jana yake.Mr.Cheo alikuwa chini ya uangalizi wa madaktari wa kutosha.Hakuruhusiwa mtu yeyote kumwona kwasababu muda wote alikuwa amelala baada ya kuchomwa sindano ya usingizi.Hata mkewe alipokwenda kumwona alirudishwa na kuambiwa aje baada ya wiki moja ndipo ataruhusiwa kumwona.Alirudi nyumbani akiwa pamoja na Mike kwa huzuni na masikitiko makubwa.
Wiki nzima jiji la Dar-es-salaam lilitandwa na polisi kila kona wakiwa katika uchunguzi wa tukio lililotokea.Mr.Cheo alitakiwa na polisi kuelezea jinsi tukio zima lilivyotokea,hivyo naye alikuwa katika ulinzi mkali. Baada ya wiki moja mkewe pamoja na Mike waliruhusiwa kumwona Mr.Cheo.
“Mume wangu nakuomba uzungumze hata maneno ya mwisho tu kwangu.Pleas I LOVE YOU!!!!”mke wa Mr.Cheo alizungumza kwa hisia zilizochanganyika na huzuni lakini mumewe hakuweza kujibu kitu chochote.Machozi yalimtiririka bila kikomo.Mike na Aunt waliamua kuondoka kurudi nyumbani.
Mike hakuweza kwenda shule kwa muda wa wiki mbili kwasababu Aunt yake alikuwa katika hali mbaya sana.Kila wakati alipoteza fahamu kutokana na mawazo juu mumewe hivyo alihitaji uangalizi wa kina.Dada yake Mike anayekaa Manzese alifika pale nyumbani ili kumsaidia Mike aweze kwenda shule.
**********************************
Je nini kitaendelea?endeleeni kugesi kwasababu hiyo iliyopita kuna baadhi ya watu walioweza kujua kitakachoendelea kwahiyo jaribu na kipande hiki mnweza mkawa ni watunzi wazuri sana kushinda hata mimi.......Mungu awabariki sana..

MTUNZI-FREDY
 mliokosa sehemu ya 9
http://j2wisdom.blogspot.co.uk/2015/01/hadithi-mwanasheria-katili-sehemu-ya-9.html

No comments:

Post a Comment