Tuesday, 18 August 2015

Baada ya kuomba radhi Basata yalitoa kifungoni shindano la Miss Tanzania.


Dar es Salaam. Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limemfungulia mwandaaji wa shindano la urembo la Miss Tanzania, Lino International Agency baada ya kuomba radhi na kufanyia kazi baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza na kutekeleza masharti aliyopewa.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo,  Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Godfrey Mngereza amesema  LINO International Agency imepewa kibali cha muda kisichozidi miezi minne kwa ajili ya maandalizi ili kukamilisha usajili wa mawakala katika ngazi husika.
Mngereza amesema kuwa mapungufu yaliyobainishwa ni pamoja na kutofuata sheria ,kanuni za uendeshaji matukio ya sanaa nchini ,kutokuwakilisha nyaraka mbalimbali za shindano lake na mikataba ya washirki,kutumia  mawakala ambao hawajasajiliwa na kupewa vibali na Baraza la sanaa la Taifa.
Amesema miongoni mwa mapungufu yaliyofanyiwa kazi na Kampuni ya Lino ni mchakato wa kusajili mawakala  na kufanyia marekebisho kanuni na taratibu za uendeshaji wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania.
chanzo:mwananchi

No comments:

Post a Comment