Monday, 24 November 2014

Hadithi MWASHERIA KATILI sehemu ya 7

 


“Jamani Mike!Mike!!Mikeeeeeeeeee!!!!!!!”wanafunzi wote walicharuka kwa vifijo na vigelegele baada ya kumwona Mike.
“Kuna nini tena huko Paredi mbona kelele hiv...yo?”Caren alimuuliza mwenzake wakiwa wanashuka kwenye basi.Gari lao lilichelewa kufika kutokana na ajali iliyotokea maeneo ya Makonde na kusababisha foleni ndefu mno.Caren alikimbia haraka pared.

Sasa endelea.......
“Mikeee!”Caren alijawa na furaha ilioje baada ya kumwona Mike akiwa mbele ya paredi akitoa monning speech.Alijikuta akimwita kwa sauti kubwa kiasi cha kuwaacha wanafunzi wenzake hoi kwa vicheko.Wakati Caren akipaza sauti yake kumwita Mike wanafunzi wote walikuwa kimya wakisikiliza speech yake.
“Thanks all,I don’t have much to say.I would like to call my friend Juma here because I hope he has something to tell you”Mike aliishiwa cha kuongea baada ya kumwona Caren.Alishuka chini mpaka kwenye mistari.Juma alipanda juu na kuwakumbusha wenzake kuhusu suala la nidhamu.Baada ya matangazo mengine toka kwa viranja na waalimu wa zamu,wanafunzi walitawanyika kuelekea darasani.
“Caren!!”
“Mike!”

kila mmoja alimwita mwenzake baada ya Caren na Mike kukutana macho kwa macho.Walikumbatiana karibu dakika tatu huku Mike akibubujikwa na machozi baada ya Caren kumuuliza mbona alikuwa haji shule.
“Nitakuelea kila kitu muda wa mapumziko,sasa hivi twende kwanza darasani.Kwani wewe upo form ngapi?”Mike alimuuliza Caren huku akiwa amemshika mkono wakichapa hatua kuelekea madarasani.
“Mimi nipo form two Green,we si upo White?”Caren alimjibu Mike kwa upole kisha akatabasamu kidogo.
“Hujakosea,ulijuaje kama mimi nipo form two White?”
“Niliambiwa na wanafunzi wengine!”
“Naona class kwenu kuna teacher,wewe nenda tutaongea baadae.”Mike alimwonesha Caren mwalimu aliyeingia darasani kwao.Waliagana kila mmoja akaelekea darasa lake.Caren alipokuwa darasani hakuelewa kilickokuwa kinafundishwa.Muda wote alimuwaza Mike na alikuwa na hamu ya kujua kilichomsibu.
Break ilipofika tu tayari Caren alikuwa mlangoni kumsubiri Mike atoke.Wanafunzi wengine walimshangaa sana Caren na kujiuliza amemjua vipi Mike wakati yeye kahamia miezi kadhaa iliyopita?Walizoeana kwa kipindi kifupi mno.Mike akiwa na rafiki zake aliondoka pamoja na Caren kuelekea Kantini ya shule kununua viti vidogo vidogo vya kutafuna.Rafiki zake Mike waliondoka na kuwaacha wawili hao wakiwa katika mazungumzo ya kina.
“Eeeeh!!hebu niambie!”Caren alimshtua Mike na kumsogelea karibu zaidi.
“Usiwe na wasiwasi”Mike alimweleza Caren yote yaliyomsibu Uncle wake na aliapa mbele ya Caren kuwa ni lazima atalipiza kisasi kwa mchungaji huyo aliyesababisha matatizo ndani ya familia yao.
“Pole sana Mike!hivi ni kweli kumbe kuna wachungaji wengine wapo hivyo?Mimi baba yangu ni mchungaji lakini hawezi kufanya mambo kama hayo.”
“Usiseme hivyo huwezi kujua siri za wazazi wako”Mike alimsihi Caren
“Hakuna cha siri hapa,mimi namjua vizuri baba yangu.Kwani huyo mchungaji anaitwa nani na kanisa lake lipo wapi?”Caren alitaka kujua jina la mchungaji huyo.
“Uncle amegoma kutuambia jina na mahali lilipo kanisa lake kwa kuwa anahofia maisha yake.Alitishiwa kuuawa endapo atatoa siri hiyo.Daah!!naona breki imekwisha twenzetu class”
Muda wa mapumziko ulikuwa umekwishi hivyo wakajikongoja kuelekea madarasani.Jioni wakati wa kutoka shule Mike na Caren walikutana tena.Caren alimwahidi Mike kuwa atakuwa naye bega kwa bega kwa kitu chochote kitakachotokea.Pia aliapa kumsaidia kulipiza kisasi kwa mchungaji aliyesababisha mvurugiko wa familia yao.
“Mimi huwa siwapendi watu wanaowasababishia wenzao matatizo,hivyo basi mchungaji huyo lazima alipe yale yote aliyoyafanya.”Caren alimweleza Mike kwa hasira hadi wanafunzi wengine waliokuwa karibu nao kumshangaa.
“Basi letu hiloo!kwaheri tutaonana kesho”Mike alimuaga Caren kisha akapanda school basi na kuondoka zake.Dakika mbili baadae basi la akina Caren lilifika naye akapanda na kuondoka.
Siku zilisonga mbele huku Mike na Caren wakisoma kwa bidii sana kwasababu walikuwa wakijiandaa na mtihani wa taifa wa kidato cha pili.Urafiki wa Mike na Caren uliendelea kukua siku hadi siku mpaka wanafunzi wengine wakaanza kuhisi ni wapenzi.
“Rafiki yangu siku hizi umenisusa kabisa”Esta aliamua kumpasulia jipu Caren.
“Siyo hivyo rafiki yangu mbona bado tupo pamoja tu!”
“Hamna sio kama zamani ulipohamia”
“Kwani mimi nimebadilika nini?”Caren alimuuliza rafiki yake Esta.
“Siku hizi naona upo closer sana na Mike mimi nimesahaulika kabisa.Umesahau kama mimi ndiye niliyekupokea ulipohamia hapa?”
“Basi kama kweli nimebadilika naomba unisamehe rafiki yangu.Mimi nipo karibu na Mike kwasababu huwa ananifundisha mambo mengi sana.”
“Mambo Esta!Caren vipi leo huendi kwenye kipindi?”
“Poa tu Mike!mbona mimi huniulizi kama naenda kwenye kipindi?au siku hizi mimi siyo rafiki yako tena?”
“Ok!i’m sorry Esta!! mambo mengi yamenichanganya mpaka nakusahau!kama vipi twenzetu teacher wenu nipo tayari.”Wote watatu waliondoka wakiwa na furaha tele mpaka darasani.Mike alikuwa na akili za ajabu sana.Aliweza kuwafundisha hadi wanafunzi wa kidato cha nne ambao nao walikuwa katika maandalizi ya mtihani wao wa taifa mwezi Octoba.
Kila walipokuwa na tatizo walimtafuta Mike na yeye bila hiyana aliwaelekeza vizuri sana.Kila mwanafunzi alimpenda Mike kwani hakuwa na majivuno.Walipenda kumpa zawadi mbalimbali kila wakati. “Nashukuru sana kwa kuonesha upendo wenu kwangu.”Mike aliwashukuru wanafunzi wenzake pindi walipompa zawadi.Mwezi Octoba kidato cha nne walianza mitihani ya taifa huku kidato cha pili nao wakiwa katika maandalizi ya mitihani yao itakayofanyika mwezi Novemba
Siku zilisonga mbele,baada ya form four kumaliza mitihani yao,wanafunzi wa kidato cha pili nao wakaanza kufanya mitihani iliyochukua takribani majuma wawili mapaka kumalizika.Baada ya mitihani shule ilifungwa na kila mwanafunzi alirejea nyumbani akiwa na furaha tele.Caren alimwelekeza Mike nyumbani kwao mitaa ya Afrikana.
“Ok.nimeshapaelewa nitakuja siku yoyote ndani ya likizo hii.Ngoja nikuandikie namba ya Aunt yangu ndio utatumia kuwasiliana na mimi”Mike alimwandikia Caren namba za simu ya Aunt yake na Caren alimwahidi kumtafuta siku za karibuni.Waliahidiana mambo mengi watakayofanya wakiwa likizo na baadae kila mmoja aliondoka kuelekea kwao.
“Mike!Mike!kuna mtu kanipigia simu kasema anakutafuta wewe.”
“Ni msichana au mvulana?”
“Ni msichana na kaniambia kuwa wewe ndio umempa namba yangu”
“Ndio Aunt naomba unisamehe sana..Mimi ndiye nimempa namba yako ili tuwasiliane,bila shaka ni Caren?”Mike alimweleza Aunt yake ukweli na kumwomba msamaha kwa kutoa namba yake bila kumjulisha.
“Haswaa Mike!kaniambia anaitwa Caren,kwani unasoma naye?”
“Ndio Aunt huyu ni mwanafunzi mwenzangu”
“Haya huyu hapa anapiga tena,chukua ongea naye”
“Asante Aunt yangu wa ukweli.”Mike alichukua simu na kuanza kuongea na Caren.Waliongea kwa muda wa dakika kumi.
“Ngoja nikupe Aunt yangu umwombe mwenyewe.Aunt!njoo anataka kuongea na wewe”Mike alimpa Aunt yake simu aongee na Caren.Baada ya kuongea Aunt akamwambia Mike…
“Nakuruhusu hiyo kesho uende huko Afrikana lakini usichelewe kurudi.Si unajua kesho ndio siku ninayoenda kumtembelea Uncle wako?”
“Nashukuru sana Aunt,nakuahidi sitachelewa kurudi na ukifika msalimie sana Uncle mwambie nitakuja siku nyingine”Usiku ulipoingia Mike akiwa chumbani kwake mara jini Bahari akamtokea.
“Nisikilize Mike tena unisikilize kwa makini sana mno”Mike alikaa kimya baada ya kusikia sauti ya Bahari “Najua kesho unaenda kwa akina Caren hivyo basi unatakiwa kuwa makini sana.Hakikisha muda wa saa saba ndio unatakiwa uwe umefika pale au zaidi ya hapo.Tofauti na hapo ukienda chini ya saa saba yatakayokupata huko usinilaumu kwa lolote lile”
“Kwani kuna nini Bahari mbona unanitisha sana?”Mike alimuuliza jini Bahari huku akiwa na hofu kubwa. “Kila siku nakwambia ukitaka mafanikio we fuata tu ninachosema.Mimi nina nia nzuri na wewe,na kama ukipingana na ninayotaka utapata matatizo makubwa sana.”
“Sawa nimekuelewa!asante sana rafiki yangu”Mike alimwahidi jini Bahari kufuata yote anayoyataka.Bahari alipotoweka Mike akaanza kuwaza..
“Sasa Caren kaniambia niwahi ili akanitambulishe kwa baba yake kwa kuwa anataka kusafiri muda wa saa tano asubuhi.Sasa sijui nifanyeje?ok.potelea mbali.Nitamwambia foleni imenichewelewesha”

Mike alipanda kitandani na kujifunika shuka baada ya kujipa moyo ni jinsi gani atajitetea kwa Caren.Palipopambazuka Mike alijiandaa tayari kwenda kwa akina Caren.Alichukua simu ya Aunt yake ambayo alishamwomba toka jana aende nayo ili kurahisisha mawasiliano.
Mike aliondoka na kumwacha Aunt yake naye akijiandaa kwenda Segerea kumsalimia mume wake Mr.Cheo.Mike alifika kituo cha daladala na kusubiri
“Ooooh!Mike habari za siku nyingi?”Mike alishtuka baada ya kusikia mtu akimwita
“Mungu wangu!!Saidi mbona kimya sana?Festo huko wapi siku hizi?”Mike alimkumbatia rafiki yake mkubwa Saidi baada ya kuonana pale kituoni.
“Mbona yupo atakuja hapa muda si mrefu.Tumepanga kwenda Kariakoo kwa babu yangu kumsalimia”
“Aaah!poa!vipi lakini skuli kunasemaje?”Mike alimtupia Saidi swali la kizushi.
“Skuli fresh tu na paper ilikuwa fresh sana .We si mkali bwana unajiamini!”Saidi alimkejeli Mike. “Eeeh!Festo huyooo!”Festo alifika mpaka walipokuwepo Mike na Saidi.Walikumbatiana kwa furaha kwa kukutana kwa mara nyingine baada ya kupotezana takribani mwaka mmoja kutokana na ubize wa shule.
“Kwani Mike unaelekea wapi?”Festo alimuuliza Mike.
“Mimi naenda Afrikana ila sina haraka sana”Mike alijibu.
“Poa basi kama huna haraka tufuatane wote mpaka Kariakoo then tutakusindikiza Afrikana.Wote kwa pamoja walikubaliana kwenda kwanza Kariakoo halafu baadae wataenda Afrikana.Daladala lilikuja wakapanda na kuondoka.
“Eeeeh!Mike nimekumbuka kitu!”Saidi alimwambia Mike wakiwa ndani ya gari
“Kitu gani tena Saidi?”
“Hivi ulishawahi kukutana na yule msichana toka tuachane naye kule Kunduchi beach mwaka jana?”
“Msichana gani tena huyo?”Festo akadakia.
“Si Caren bwana!kwani humkumbuki?”
“Ok.kweli nimeshakumbuka,Mike hebu tueleze kinagaubaga”
Mike alitabasamu kidoga kisha akakohoa kutengeneza koo lake “Yaani washikaji ilikuwa kama zali kwangu.Huwezi kuamini,yule msichana mbona kahamia skuli kwetu tangu January!lakini nilimwona mwezi wa saba!”
“Kweli mwanangu hilo zali,sasa mbona unatuchanganya tena unavyosema ulimwona mwezi wa saba,kivipi?”Festo na Saidi wote walimshangaa Mike.
“Mimi tangu January sikuwepo shule,nilikuwa tu nyumbani kwa kukosa ada”
“Unasema ulikosa ada!kwani Unlce wako aligoma kukulipia au?”
“ Siyo hivyo”Mike aliwasimulia rafiki zake matatizo yote yaliyomkumba Uncle wake”
“ Pole sana Mike!”walimpa pole nyingi na vile vile walimtia moyo. Walifika Kariakoo majira ya saa nne asubuhi.Walishuka na kuanza kukata mitaa kuelekea mtaa wa Kongo anapoishi babu yake Saidi.Mara simu ya Mike ikaita..
“Hello!!mimi ndio natoka home,kulikuwa na kazi kidogo hapa nyumbani,wala usijali nitawahi kabla hajaondoka”Mike alipomaliza kuongea simu ilikatika.
“Nani huyo Mike unayemdanganya eti ndio unatoka home?”Saidi alimchokoza Mike
“Huyu ni Caren,ndio nilikuwa naelekea kwao Afrikana.Aliniambia niwahi kabla ya saa sita niwe pale ili akanitambulishe kwa baba yake ambaye atasafiri leo hii majira ya saa saba kwenda sijui Nigeria!sijui Algeria?hata sikumbuki vizuri”
“Sasa si ungetuambia tukuache uende”Festo aliamua kumfokea Mike.
“Hapana sio hivyo!mimi sitaki kuonana na baba yake.We si unajua watoto wa kishua unaweza kupigwa risasi bure!”
“Kweli mtu wangu utaenda baadae”
“Lakini atamaind kinoma!”Mike alitania
“Potelea mbali ilimradi usidhurike bwana!mbona hutufiki!we Saidi au umepasahau kwa babu yako?”Festo alishindwa kuvumlia
“Tumeshakaribia mtu wangu ni hapo tu kwenye hiyo kona”Baada ya hatua kumi walifika kwa babu yake Saidi na walikaribishwa vizuri sana.Walimsalimia babu na kuzungumza naye mambo mengi.
Saa sita na nusu mchana waliondoka kuelekea Afrikana.Simu ya Mike ilishapigwa karibu mara sita na Mike alimweleza Caren ukweli kuwa hatoweza kuwahi kwani foleni ilikuwa ndefu sana.Walipofika Mwenge walikutana na baadhi ya magari kama kumi yakiwa yamewashwa taa zote za mbele.
“ Kwani kuna mheshimiwa yeyote anayepita leo?”Mike aliamua kuwauliza wenzake baada ya kuyaona magari hayo.
“Hebu kwanza!!aaaaah!haya ni magari ya Pasta Ndundu,mbona unashangaa kwani humjui?ana kanisa kubwa tu maeneo ya Kimara linajulikana karibu Dar nzima”
“Nimeshagundua kitu!”
“Kitu gani umegundua wewe?au unafikiri huyu ndiye aliyemharibia Uncle wako nini?”Saidi alikurupuka na kumshangaa Mike aliposema amegundua kitu.
“No!wala siyo hivyo!kama ni Pasta Ndundu basi huyu ndiye baba yake Caren na hapa unapomwona ndio anaondoka zake.Aliniambia atasafiri mida hii”
“Ha!ha!ha!ha!sasa kama baba yake ni mchungaji wewe uliogopa nini?Mapasta huwa hawana neno”Saidi aliamua kumcheka Mike kutokana na uoga wake.
“Wangejua jinsi nilivyokuwa na hamu ya kumwona baba yake,wala wasingeongea haya.Kama siyo Bahari we acha tu!!!”Mike alijisemea mwenyewe kimoyomoyo.
“Oya !konda shusha Afrikana hapo chukua nauli yako kata watatu”Mike alilipa nauli kisha wakashuka na kuanza kumtafuta Caren kwenye simu. “Hello!tupo hapa kituoni njoo basi”Festo alinunua mahindi ya kuchoma wakawa wanatafuna huku wakimngojea Caren.Baada ya dakika kumi Caren aliwasili kituoni.
“Waoooh!!Saidi,Festo habari za siku nyingi?”Caren alifurahi zaidi kuwaona rafiki zake Mike.Walisalimiana na baadae walianza safari ya kuelekea nyumbani kwa akina Caren.
“Leo umeniudhi sana Mike!”
“Kwanini Caren,kwani nimefanya nini?”
“Mimi si nilikwambia uwahi kabla baba yangu hajaondoka,sasa wewe umefanya nini?”
“Sorry sana Caren kulikuwa na shughuli naifanya pale home isitoske foleni pia imechangia,ila usijali akirudi nitamwona tu”
“Yes.ameondoka muda si mrefu”
“Kwanza tumekutana nae hapo Mwenge”Mike alijaribu kujitetea mbele ya Caren.
“Unasema umemwona kwani unamjua?”Mike alipata swali toka kwa kimwana mwenye uzuri wa asili.
“Akina Festo ndio wameniambia kuwa yale magari meusi ni ya Pasta Ndundu.Kuna magari ambayo yalitupita yakiwa yamewashwa taa zote za mbele.”
Mike alimjibu Caren kwa ufasaha zaidi.
“Karibuni hapa ndio nyumbani!”Caren alifungua geti la nyumba yao na kuwakaribisha rafiki zake.Waliwahi kufika kwasababu sio mbali sana na kituo cha daladala.
Waliingia mpaka sitroom na kuketi,nyumba ilikuwa ya kifahari sana. “Mama!mama!njoo uwaone rafiki zangu wamefika!”Caren alimwita mama yake na mara moja aliwasili.
“Hamjambo wanangu?”
“Hatujambo shikamoo mama!”Wote walimsalimia mama Caren kwa heshima.Caren aliwatambulisha kila mmoja kwa jina lake.
“Nashukuru kwa kuwafahamu wanangu.Mimi nipo ila baba yake mwenzenu amesafiri muda si mrefu kwenda Nigeria nafikiri atarudi mwakani.Atakaa huko mwezi mzima akiendesha shughuli zake.”
“Kwahiyo mama Chrismass mnakula wenyewe bila baba kuwepo?”Mike aliuliza swali la kichokozi.
“Ha!ha!ha!ni kweli mwanangu ila tumeshazoea”Kitambo kidogo kilipita mazungumzo yakiendelea. “Nenda kawaletee wenzako chakula”Caren aliagizwa na mama yake kwenda kuwaletea wenzake chakula.Baada ya akina Mike kula chakula story ziliendelea mpaka jioni ndipo waliaga na kuondoka kurudi nyumbani.
Mwezi Decemba ulipita vizuri kwa Mike na Caren.Kila mmoja alisheherekea sikukuu za Chrismass na mwaka mpya kwa furaha na amani.Mwezi January matokea ya kidato cha pili yalitoka.Mike aliwashangaza wanafunzi na waalimu kwa kushika nafasi ya kwanza kwa Wilaya ya Kinondoni huku akiwa amekosa vipindi vya muhula mzima wa kwanza.
Waalimu pamoja na wanaafunzi wenzake walimpongeza sana.Mwenye shule aliamua kumfanyia tafrija ndogo hapo hapo shuleni,pia aliamua asome bure katika shule yake mpaka atakapomaliza kidato cha nne.Mike alifurahi sana ,akabubujikwa na machozi ya furaha.Alitamani Uncle angekuwepo kwenye tafrija hiyo.Caren naye alifaulu kwa wastani mzuri kiasi.

***********************
Je nini kitaendelea baada ya hapo?Usikose toleo lijalo ambalo litakuwa tamu zaidi ya haya yaliyopita....Nawashukuru sana kwa kufuatilia hadithi hii na Mungu awabariki sana...Nawatakia siku njema.

*****************
Kwa maoni au ushauri Anapatikana kwa namba 0655089197/0766123623

MTUNZI-FREDY MZIRAY

No comments:

Post a Comment