Tuesday, 18 November 2014

Nape:Chagua CCM chama kinachoweza kuleta maendeleo na kutatua kero zinazowakabili.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye (pichani), amesema maendeleo kamwe hayawezi kupatikana kwa njia ya matusi na kufarakanisha wananchi kama wanavyofanya viongozi wa upinzani.

Pia amewataka wananchi kuhakikisha wanachagua wagombea wa CCM katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa akisema ndicho chama chenye viongozi imara watakaowaletea maendeleo.

Nape aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa kata ya Chumo wilayani Kilwa na kwamba kazi ya CCM ni kuhakikisha inashirikiana na wananchi katika kuwaletea maendeleo tofauti na wapinzani ambao kazi yao ni matusi na kufarakanisha wananchi.


Alisema wananchi wasichague vyama vya upinzani kwa sababu havina lengo la kuwaletea maendeleo, badala yake wachague CCM kwa kuwa ndicho chama kinachoweza kuwaletea maendeleo na kutatua kero zinazowakabili.

“Hakuna maendeleo yanayoweza kuja kwa njia ya matusi , ahadi hewa wala kukejeli kazi zinazofanywa za kuwaletea wananchi maendeleo, kazi ya kutukana na kukejeli ni ya wapinzani na CCM kazi yake ni kuboresha maendeleo ya wananchi,” alisema.
nipashe

No comments:

Post a Comment