“Sasa Pasta Ndundu huyu jamaa keshajua mambo yako mengi na ni lazima atatoa taarifa hizi polisi.Chamsingi hapa tummalize kabla hajafika mbali au unaonaje mheshimiwa?”kijana mmoja alim...shauri bosi wake baada ya Mr.Cheo kuondoka eneo lile.
“Hapana haina haja ya kumuua,mimi nina plani nyingi za kumharibia maisha yake.Mimi ndio Pasta Ndundu bwana hawezi kunichafulia jina.Kwani humkumbuki Mr.Chazi mpaka leo yuko jela? Alijifanya anaweza kuachana na dili zangu kirahisi ili akanitangazie! Lazima ataozea jela”
“Nakuaminia bosi wangu, pesa ndo kila kitu” kijana aliyekuwa karibu na Pasta Ndundu alimpongeza bosi wake “Sasa ni njia gani tutatumia ili tuweza kumsweka ndani?”
“Wewe ondoka sasa hivi mfuatilie popote atapokwenda kwa gharama yoyote.Hakikisha unamjua huyo anayemuuzia bidhaa na mahali anapoishi, sawa?”
“Sawa!! bosi usihofu”
“Nenda sasa hivi kabla hajafika mbali”Pasta Ndundu alimpa kijana wake kazi ya kumfuatilia Mr.Cheo. Mr Cheo aliondoka bila kujua kama anafuatiliwa na mtu.Alifika mpaka hotelini alipofikia,kisha akaoga na kubadilisha nguo.
“Hello! niandalie tiketi ya usiku huu” Mr.Cheo alipiga simu uwanja wa ndege na kuomba tiketi ya kusafiria usiku huo huo.
“Ngoja nisogee karibu zaidi naona anapiga tena simu” Jamaa yule anayemfatilia Mr.Cheo alijisemea mwenyewe kimoyo moyo na kusogea karibu zaidi na dirisha kusikiliza.
“Hello!Mr.a’m coming right now because I want to go back at home this night.Don’t worry you will be send to me day after tomorrow,ok see you leter” Mr.Cheo alimaliza kuongea kisha akakata simu
“Atakuwa anaenda kulipia bidhaa zake. Yes! kazi imekuwa rahisi kidogo”Jamaa yule alifurahi sana kwa kuwa aliamini kazi yake itaisha siku ile ile.Alijificha nyuma ya tanki kubwa la maji na kumsubiri Mr.Cheo atoke.Baada ya Mr.Cheo kutoka aliingia ndani ya gari na jamaa aliwasha pikipiki yake na kuanza kulifuatilia gari aliondoka nalo Mr.Cheo
Alishuka mtaa mmoja hivi mjini Abuja kisha akaingia godauni moja. Alikaa huko kwa muda kama wa nusu saa hivi.Baada ya hapo aliondoka kuelekea uwanja wa ndege kuhakikisha kama tiketi iko tayari.Usiku wa saa mbili Mr.Cheo alipanda ndege kuelekea Dar es salaam akiwa na mawazo tele juu ya vitisho alivyopata toka Pasta Ndundu
Aliapa kutomwambia mtu yeyote yule juu ya yale aliyoyaona. “Pasta Ndundu kazi imekamilika,nimeshapajua anaponunua mizigo yake”Kijana aliyetumwa na Pasta Ndundu kumfuatilia Mr.Cheo alimpigia bosi wake simu kumjulisha kuwa ameshafanya kama alivyomwagiza
“Yes!good boy!wewe rudi hapa hotelini nikupe maelekezo na plani ya kufanya.Fanya haraka sana” Pasta Ndundu alimpongeza kijana wake kwa kazi nzuri aliyoifanya.Pasta Ndundu alikutana na vijana wake na kuanza kupanga namna ya kummaliza Mr.Cheo.
“Nisikilizeni kwa makini sana,kesho asubuhi tutaenda mpaka pale kwenye ilo godauni na tutanunua bidhaa kama wateja wengine kisha tutamwambia muuzaji autume huo mzigo pamoja na mizigo ya Mr.Cheo kwa sababu yeye ataipokea yote Dar es salaam
“Wakati wa kwenda tunaenda na yaha mabox ya madawa kisha tunayachanganya na mizigo hiyo,then mimi nitamaliza mchezo”Walikubaliana vizuri kisha kila mmoja akaendelea na shughuli zake.Kesho yake asubuhi Pasta Ndundu aliwaamuru vijana wake waweke mizigo ya madawa kwenye gari.Baada ya kutekeleza amri hiyo gari liliwashwa wakaondoka kwenda kwenye godauni walilotaka kwenda.
“Good morning”Pasta Ndundu alimsalimia yule muuzaji iliyemkuta.Baada ya salamu alianza kununua bidhaa mbalimbali kisha akamweleza kila kitu kama walivyopanga na vijana wake.Mbaya zaidi alimdanganya kuwa eti alikuwa pamoja na Mr.Cheo ila yeye aliamua kutangulia kutokana na dharura aliyoipata.
“These are another goods,put together with those”Pasta Ndundu alimpa yale mabox ya madawa na kumwambia yanakwenda pamoja na mizigo yao.Walikubaliana kuwa atarudi kesho yake ili amsaidie kusafirisha.Alimpatia fedha za kutosha na kumwahidi kuwa atakuwa mteja wake wa kudumu.Pasta Ndundu aliondoka na vijana wake wakiwa na furaha tele.
Asubuhi siku iliyofuata Pasta Ndundu akiwa na vijana wake walichukuwa ile mizigo pamoja na muuzaji kuelekea uwanja wa ndege. “Oooh!Pasta how are you?”
“A’m fine what about you?”
Pasta Ndundu alisalimiana na askari wa pale uwanja wa ndege.Pasta Ndundu alijulikana mno katika uwanja wa ndege wa Abuja,si wakaguzi au wafanyakazi wa mashirika ya ndege,wote walimjua kutokana na kusafirisha mizigo ya magendo mara kwa mara.Alisifika kwa kuhonga fedha nyingi mpaka ikafika hatua ya mizigo yake kutokaguliwa,yeye akifika ni kutoa fedha tu!
Aliwapatia wale askari pesa kisha akaingia ndani.Pia aliwapatia wakaguzi fedha na mizigo ikaenda moja kwa moja mpaka ndani ya ndege.Yule muuzaji alishangaa mno,alipewa fedha nyingine na Pasta Ndundu kisha wakaagana na kuondoka zake.Baada ya saa moja na nusu ndege ilipaa kuelekea anga la Nairobi na baadae ardhi ya Dar-e s- salaam.
“Nafikiri tumemaliza kazi sasa twendeni tikale raha!”Pasta Ndundu alikuwa na furaha iliyopitiliza.
“Lakini sio vizuri tulivyofanya jamani!kumsingizia mtu kesi?”kijana mmoja kati yao alimwonea huruma Mr.Cheo kwani aliona hakuwa na kosa lolote.
“Huyu mpumbavu nini?kama hutaki kazi sema tena utaishia pabaya sana.Halafu nina wasiwasi ipo siku utanisaliti nyang’au mkubwa wewe”Pasta Ndundu alifoka kwa hasira.
“Ok.nisamehe bosi wangu siwezi kukusaliti,nilikuwa nakutania tu mkubwa wala usihofu tupo pamoja”kijana yule alijaribu kujitetea.
“Utani gani huo wa kijinga ninaweza kukupoteza muda wowote ule,unacheza na mimi!!”
“Basi bosi msamehe tu ameomba radhi”kijana mwingine alimwombea mwenzake msamaha.
“Ok.nimemsamehe haya twendeni”Pasta Ndundu alimsamehe yule kijana kisha wakaondoka eneo lile.Jioni Pasta Ndundu alipiga simu uwanja wa ndege wa Dar-es-salaam na kuwajulisha kuwa kuna mzigo wenye madawa ya kulevya unaingia nchini kupitia ndege ya mzigo ya Kenya air way.
Polisi jijini Dar-es-salaam walijiandaa kikamilifu pale uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere wakiisubiri ndege ambayo ilitarajiwa kutua majira ya saa nne usiku.Ilichelewa kufika kutokana na kupata itilafu ilipofika Nairobi na kuwa katika matengenezo ya kina.
Toka saa moja usiku wakaguzi wa mizigo walikuwa tayari wameshajiandaa na vifaa vyao vya ukaguzi.Simu zilipigwa kila wakati ili kupata uhakika wa ndege hiyo kama itatua muda huo au la!Taarifa walizozipata ni kwamba wakae tayari kwasababu ndege itatua muda wowote.
Haukupita muda mara ndege ikaanza kuambaambaa angani na kufungua matairi yake tayari kwa kutua.Dakika mbili mbele ndege ya mizigo ya shirika la Kenya air way ilitua mjini Dar-es-salaam.
“Helo!helo!kwa yeyote mwenye mizigo ndani ya ndege hii hatutaruhusu kuchukuliwa kwa mzigo wowote ule mtakuja kesho asubuhi.Kuna ukaguzi wa kina unafanyika ndani ya ndege hii.Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza lakini hii ni kwa usalama zaidi.”
Tangazo lilitolewa chumba cha matangazo pale uwanjani kuwataarifu wafanyabiashara waliokuwa wanasubiri mizigo yao.Baada ya tangazo hilo watu walianza kuondoka mmoja mmoja na baadae pakawa shwari kabisa.Ukaguzi ulianza kufanyika mzigo mmoja baada ya mwingine.
“Ok.angalia nembo hii ni ya nani kwenye kitabu cha wasafiri?”Askari mmoja alimwambia mfanyakazi wa ndege hiyo baada ya kupekua mabox fulani hivi!Baada ya kuangalia vizuri ile nembo yule mfanyakazi wa ndege akasema….
“Hiyo ni mizigo ya Mr.Cheo”
“Nashukuru sana kaka,angalia anaishi wapi na nyumba namba ngapi?”
“Anaishi Ubungo Plaza nyumba namba 0037”
“Pumbavu sana huyu ndiye anayeingiza madawa ya kulevya nchini?”Waliendelea na ukaguzi wa mizigo mingine,baada ya kumaliza zoezi zima la ukaguzi waliondoka.Kesho yake asubuhi walitumwa askari kwenda kumkamata Mr.Cheo.Baada ya ushahidi wa kesi yake kukamilika alitupiwa lupango miaka 15.
*************************
Je nini kitaendelea?usikose sehemu ijao yenye mambo mazuri zaidi ya haya....Nashukuru sana kwa ufuatiliaji wako..

MTUNZI-FREDY MZIRAY
No comments:
Post a Comment