Monday, 5 January 2015

Hadithi-MWANASHERIA KATILI SEHEMU YA 9


Mwaka mmoja sasa tangu Mr.Cheo afungwe jela.Kila wakati alilia sana kwa uchungu kutokana na kubambikiziwa kesi tena na mtu anayetegemewa na jamii kuwaongoza kiroho.Kila akiikumbuka familia yake machungu yalizidi,biashara zake zote zimekufa,nyumbani wamefilisika.
“Futa machozi Mr.Cheo hii ndio dunia.Si kila anayefungwa ana makosa wengine wanasingiziwa kama wewe.”Mfungwa mwenzake Mr.Cheo alimfariji.
Alikumbuka alipokuwa na familia yake japokuwa hakubahatika kupata mtoto toka alipofunga ndoa,lakini alimpenda sana Mike pamoja na dada zake na ndugu zake kwa ujumla.Ilikuwa kama sinema kwenye kichwa chake kwani aliona alivyokuwa na Mike wakitaniana pale sitroom.Mkewe alikuja na kumkumbatia,chakula kizuri alikula kilichoandaliwa na mke wake kipenzi.Machozi yalimbubujika baada ya kuliona lango kuu la gereza likifunguliwa,alishahisi yupo nyumbani kumbe sivyo.
“Twendeni!twendeni!”Askari aliwatangazia wafungwa wote kuwa wanatakiwa kwenda shambani kulima.Karandinga lilikuja kisha wakapanda wakiwa na majembe mkononi tayari kwenda kulima.Walipofika shambani walianza kazi mara moja.Mr.Cheo alilima karibu na mfungwa mmoja mwanamke ambaye alionekana kachoka sana.
Dakika mbili mbele yule mwanamke alianguka chini. “Inuka ulime kabla sijakumaliza.”Hayo ni maneno ya askari mmoja akimwambia yule mwanamke.Alitoa rungu lake na kuanza kumpiga.

“Naumwa nisaidieni jamani!!!!nakufaa!!”Sauti hafifu ilitoka kwa yule dada akiomba msaada lakini aliendelea kupigwa mpaka akaanza kutapika damu.
“Mungu wangu!huyu askari anafanya nini?mtu anaumwa yeye anaendelea kumpiga tu!”Mr.Cheo alimwonea huruma sana yule mwanamke.Alinyanyua jembe na kumpiga yule askari kichwani.Askari alianguka chini na kuanza kuvuja damu mfululizo.
Walikuja askari wengine na kumshambulia Mr.Cheo kama mwizi.Maskini ya Mungu Mr.Cheo alipigwa mpaka akapoteza fahamu,damu zilimtoka mwili mzima.Walichukuliwa wote watatu yaani Mr.Cheo,askari aliyepigwa na jembe kichwani pamoja na yule mwanamke mgonjwa wakapelekwa hospital ya gereza.
Hali iliendelea kuwa mbaya sana kwa Mr.Cheo hadi ikafikia hatua ya kuhamishiwa hospital ya Muhimbili.Alitibiwa kwa muda wa wiki mbili,taratibu akaanza kupata nafuu ya mwili lakini alishindwa kuongea.Mke wa Mr.Cheo aliendelea kumtembelea mumewe kama kawaida yake kule garezani lakini safari hii aliambiwa kuwa Mr.Cheo ni mgonjwa yupo hospitalini ila haruhusiwi mtu yeyote kumwona kwasababu yuko chini ya ulinzi mkali.
Alihuzunika mno ikawa ni kilio kila wakati.Ni jambo la kawaida sana katika hospitali ya Muhimbili kutembelewa na viongozi mbalimbali wa dini kwaajili ya kuwaombea na kuwafariji wagonjwa.Siku moja alikuja mchungaji mmoja maarufu sana jijini Dar-es-salaam.Aliwasalimia wagonjwa na kuwaombea kila chumba.
Aliingia moja kwa moja hadi chumba alichokuwa amelazwa Mr cheo kwa lengo la kumpa neno la kiroho “No;Pasta Ndundu;Pasta feki, mwongo huyo,anafanya biashara haramu ya madawa ya kulevya. Amenisingizia kesi ,mwongo huyu!!”
Mr. Cheo aliongea kwa sauti kali baada ya kumwona Pasta Ndundu aliyeingia pale kwaajili ya kuwaombea wagonjwa. Askari na Manesi walishanga sana kwani ni muda umepita sasa Mr.Cheo alikuwa hawezi kuongea.Pasta Ndundu naye alihamaki alipomuona Mr.Cheo katika hali ile.
“Mchungaji vipi unamfahamu huyu mgonjwa?”Msaidizi wake Pasta Ndundu alimuuliza swali hilo
“Shindwa pepo mchafu!huyu anaonekana ana mapepo,anahitaj maombezi zaidi,hivyo twendeni tutarudi tena kesho”Pasta Ndundu aliweleza wasaidizi wake na kuanza kuondoka.
“Mimi nasema kweli sina mapepo wala nini mwongo mkubwa huyo!mshirikina kwanza” Mr.Cheo aliendaelea kuongea kwa sauti ya unyonge.Nesi alienda kumchoma sindano ya usingizi na mara moja akalala. Pasta Ndundu aligoma kuendelea na maombiezi vyumba vingine na kuamuru warudi nyumbani mara moja.
Baada ya kufika nyumbani Pasta Ndundu aliwapigia simu kundi la vijana fulani na kuwataka wafike nyumbani kwake na mara moja walitii amri. Walikuwa vijana wanne,waliingia ndani na kumkuta Pasta Ndundu peke yake ndani ya nyumba.
“Naam bosi! tumekuja kuna tatizo gani?” Mmoja kati ya wale vijana aliuliza
“Ketini kwanza ili niwaeleze” Pasta Ndundu aliwataka wale vijana wakae kwanza kisha akaanza kuwapa majukumu. “Nisikilizeni kwa makini sana,nataka muende moja kwa moja mpaka hospitali ya Muhimbili sekta ya kutibu vidonda ,ghorofa ya nne chumba namba 104 mtamkuta mgonjwa mmoja amefungwafungwa mwili mzima kisha kateni ulimi wake wala msimuue”
“Sawa bosi “
“Kuweni makini sana pale kuna askari wanamlinda, wakiwashinda nyie pigeni risasi tu then fanyeni kama nilivyowambia.Ulimi ndio umemponza,huyu anataka kunichafulia jina”Wale vijana waliondoka mpaka Manzese . Waliingia nyumba moja hivi iliyopo ndani ndani sana.
Walipofika ndani mmoja alifungua chumba kingine na kutoa bunduki tatu na bastola moja,pia alitoa box la risasi na kujaza kwenye bunduki zao.
“Tunaenda muda wa saa nne usiku, kazi tunafanya robo saa tu au siyo?”
“Hamna noma sisi ni makamanda bwana”Wale vijana walijadili mbinu za kuingia pale hospitali mida ya usiku.
Walichora ramani ya hospitali kisha wakaamua kuwa mmoja wao atajifanya mgonjwa mahututi hivyo anahitaji huduma ya haraka sana then watamaliza mchezo.Saa tatu usiku Black Chata na wenzake waliwasha gari na kuanza safari ya kuelekea Muhimbili hospitali . Black Chata ni jina la kijana mmoja kati ya wale wanne waliotumwa na Pasta Ndundu.
Vijana hawa walijihusisha na usambazaji wa madawa ya kulevya jijini Dar-es-salaam,kwa hiyo kazi za hatari kwao ni jambo la kawaida sana.Kwa kuwa usiku huwa hakuna foleni barabarani haikuchukua muda mrefu tayari walishafika Muhimbili.Geti lilifunguliwa wakaingia mpaka ndani.Walishuka haraka haraka na kumtoa mgonjwa wakaenda mpaka mapokezi.
“Kuna mgonjwa wetu anaumwa sana anahitaji matibabu haraka.”Waliuguzi walikuja na kumbeba mgonjwa kwenye kitanda cha magurudumu na kuanza kukisukuna kuelekea ndani.
“Nyie subirini hapo hamruhusiwi kuingia ndani usiku huu”Nesi mmoja wa zamu aliwaambia akina Black Chata na wenzake kusubiri nje.Black Chata alifunua koti lake kubwa na kumwonesha yule Nesi bunduki
“Nyamaza hivyo hivyo!ukithubutu kufungua mdomo wako umekwisha,sasa fuata maelekezo ninayokupa.Tupeleke moja kwa moja mpaka alipopelekwa mgonjwa wetu kisha mengine yatafuata”
“Sawa twendeni”yule Nesi alitetemeka sana hadi akashindwa kuongea.Waliondoka wote wanne mpaka chumba cha mahututi ghorofa ya tatu.
“Wote kimya!”sauti nzito ya ukali iliwaamrisha wale wauguzi.Walishangaa kumwona mgonjwa akiinuka mwenyewe toka kitandani kisha akatoa bastola kwenye mfuko wa koti lake.
“Ok.tunatakiwa tufuatane wote mpaka ghorofa ya 4 chumba namaba 104.”Waliondoka wale vijana,wauguzi pamoja na yule Nesi mpaka chumba alicholazwa Mr.Cheo.Walipofika mlangoni waliweka bunduki zao silent kisha Black Chata akauliza…
“Kuna askari wangapi humu ndani?”
“Wapo wawili tu!”mmoja wa wauguzi alijibu.
“Poa!ingieni kwanza nyie!”Wauguzi walitangulia kuingia ndani kisha wale vijana wa kazi wakafuata nyuma.Waliwakuta askari wakila chakula.
“Niger action!”Black Chata alimwamuru mwenzake anayeitwa Niger.Mara Niger akatoa bunduki yake na kuwashuti wale askari.Walianguka chini na damu zikatapakaa kila mahali.
Wauguzi walitetemeka sana baada ya kuona askari wameuawa.Mr.Cheo kwa muda huo alikuwa amelala fofofo!wala hajui kinachoendelea.
**************************
Je nini kitaendelea baada ya majambazi kuingia chumba alicholazwa Mr Cheo na kuwaua askari wote waliokuwa wanamlinda?hebu jaribuni kugesi kwenye comment zenu pengine na wewe unaweza ukawa ni mtunzi mzuri bila kujijua....
MTUNZI-FREDY MZIRAY

MLIOKOSA SEHEMU YA 8 BOFYA HAPO CHINI
http://j2wisdom.blogspot.co.uk/2014/12/hadithi-mwanasheria-katili-sehemu-ya-8.htm

No comments:

Post a Comment