Monday, 29 April 2013
THE BEST PHOTOS OF DAY MARTIN KADINDA AND WEMA SEPETU
Baba mzazi adaiwa kumbaka na kumsababishia maumivu BINTI yake
Morogoro. Polisi mkoani Morogoro wanamshikilia mkazi wa mjini hapa kwa tuhuma za kumbaka na kumsababishia maumivu makali mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka minane mwanafunzi wa darasa la kwanza.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa, John Laswai alisema kuwa tarehe na muda usiofahamika mwanaume huyo kwa muda mrefu alikuwa akimwingilia kimwili mtoto wake huyo anayesoma katika shule ya msingi.
Laswai alisema kuwa mwanaume huyo siku ya tukio alimwingilia mtoto wake, lakini kabla ya kufanya kitendo hicho alimtuma mtoto wake wa kiume ambaye ni bubu mwenye umri wa miaka 13 dukani mtoto huyo aliporudi alikuta baba yake akitaka kumfanyia unyama huo mdogo wake ndipo alimsadia na wakati wakitaka kukimbia baba alimshika mtoto wa kike na kumfungia ndani.
'Vurugu nchini raia wamekata tamaa'
Wakati vitendo vya wananchi kujichukulia sheria mikononi vikiendelea kushika kasi nchini, mwanasaikolojia ameeleza kwamba vinachangiwa na hasira za muda mrefu kiasi cha kuwafanya watu kukata tamaa.
Aidha, mwanasaikolojia huyo, Dk. Kitila Mkumbo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ameeleza pia kwamba kukata tamaa huko (frustration) kunachangiwa na hali ya wananchi kutonufaika na rasilimali za nchi yao kwa kipindi kirefu.
Alisema hasira za muda mrefu kwa wananchi dhidi ya vyombo vya dola hususani Jeshi la Polisi pamoja na uvunaji wa rasilimali usiowanufaisha, unachangia 'uasi' wa wananchi unaosababisha kujichukulia sheria mkononi.
“Kila tukio (la kujichukulia sheria mkononi), lina maana yake. Ukiangalia kule Liwale ni korosho, Loliondo ni ardhi, Mtwara ni gesi, mauaji ya polisi kama kule Ngara na Rufiji ni hasira dhidi ya kutotendewa haki na vyombo vya dola na yote hii ni hasira za muda mrefu,” alisema.
Alex Massawe mtegoni nchini Afrika Kusini
Dar es Salaam. Mfanyabiashara maarufu Alex Massawe ameingia kwenye mtego wa Polisi wa Afrika Kusini ambao wamekuwa wakimsaka baada ya kuombwa na Serikali ya Tanzania.
Habari kutoka katika Jeshi la Polisi zinaeleza kuwa baada ya Polisi wa Tanzania kuthibitishwa na maofisa wa Afrika Kusini kuwa wamefahamu aliko wameandaa maombi kwenda Shirika la Polisi la Kimataifa (Interpol) ili akamatwe na kurejeshwa nchini.
Licha ya kutokufahamika kwa sababu za kusakwa kwake, hakuna kiongozi yeyote wa polisi aliyekuwa tayari kuzungumzia tukio hilo lakini chanzo cha kuaminika kutoka katika jeshi hilo kilieleza kuwa wenzao wa Afrika Kusini wamewaeleza kuwa wamefahamu aliko.
Kusakwa kwa Massawe kumezua maswali kadhaa kutokana na kutokuwekwa wazi. Lakini Aprili 4, mwaka huu alitajwa mahakamani katika kesi ya mauaji ya mfanyabiashara Onesphory Kituly ambaye aliuawa katika mazingira ya kutatanisha Novemba 6, 2011 akiwa nyumbani kwake Magomeni, Dar es Salaam.
Siri nzito sakata la Lema
TUKIO la kukamatwa na kuwekwa mahabusu kwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), kwa madai ya uchochezi, limeibua sura mpya baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutajwa kuwa nyuma ya mkakati huo, Tanzania Daima Jumapili limedokezwa.
Lema ambaye bado anaendelea kusota rumande siku ya tatu baada ya kunyimwa dhamana, ameanza kufanyiwa vituko na Jeshi la Polisi baada ya jana asubuhi mkewe kuzuiliwa asimpe mswaki wala chai.
Lema ambaye bado anaendelea kusota rumande siku ya tatu baada ya kunyimwa dhamana, ameanza kufanyiwa vituko na Jeshi la Polisi baada ya jana asubuhi mkewe kuzuiliwa asimpe mswaki wala chai.
Friday, 26 April 2013
Wabunge hivi mnaridhika na Khanga Moko?
Khadija Kalil
Au baada ya salaam, msomaji wangu ikiwa waheshimiwa wabunge la Jamhuri ya Muungano wanaendelea na mikutano yao huko Dodoma, wakizungumzia mambo mbalimbali yanayohusu mustakabali wa nchi, nina ujumbe kwa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Ikiwa ndiyo wizara mama ya masuala yanayohusu michezo, utamaduni na vijana, nawaomba kwa mara nyingine tena, watupie macho makundi ya sanaa yanayovunja maadili ya utamaduni wa Mtanzania.
Uvunjwaji wa maadili unaofanywa na makundi hayo, hivi sasa unazidi kuota mizizi na kunawiri kila kukicha, huku wahusika wakionekana kufumbia macho licha ya vilio vingi kutaka hatua zichukuliwe.
Makundi kama Khanga Moko ‘Laki Si Pesa’, Kitu K na mengine yanazidi kujizolea ‘sifa’ kuvunja maadili ya Kitanzania katika maonesho yao mbalimbali.
Waheshimiwa wetu mnapokutana mjengoni, burudani nyingi tunatarajia zitaletwa huko, lakini kuna makundi mengine mnapaswa kuyakemea kwa nguvu zote na siyo kwa kuiachia wizara pekee.Ray: Siumwi jamani
MWIGIZAJI na muongozaji wa filamu, Vincent Kigosi ‘Ray’ ameamua kuvunja ukimya na kudai kwamba kupungua kwake mwili sio kwamba anaumwa bali ni katika kubadilisha muonekano wake.
Akifunguka katika kipindi cha ‘Action Cut’ kinachorushwa na Chanel Ten, Ray alisema kumekuwepo na maneno mengi yanasemwa na watu na mengine kumfikia kuwa kuna kitu kinamuuma, hivyo ni bora aombe msaada mapema ili aweze kusaidiwa.
“Jamani nataka kuwahakikishia mashabiki wangu kuwa sina panaponiuma bali nimeamua
kuutengeneza tu mwili wangu kama wafanyavyo mastaa wa nje na kutokana na hali hii, sasa hivi naweza kucheza nafasi mbalimbali, ikiwemo kupigana, mwanafunzi na wategemee kuniona katika aina nyingine ya uigizaji na siyo ile waliyonizoea,” alibainisha Ray.
chanzo:daima
‘Gereza kama boma la mbuzi’
Dodoma. Mbunge wa Kibaha Mjini, Silvestry Koka (CCM), amelifananisha Gereza la Mkuza kuwa sawa na boma la mbuzi na hivyo, halifai kutumika kwa maisha ya binadamu.
Koka alitoa kauli hiyo kupitia swali lake la nyongeza bungeni ambapo alisema hali ya gereza hilo si ya kuridhisha na linatia aibu kuwaweka binadamu.
Koka alitoa kauli hiyo kupitia swali lake la nyongeza bungeni ambapo alisema hali ya gereza hilo si ya kuridhisha na linatia aibu kuwaweka binadamu.
“Kutokana na idadi kubwa ya wafungwa na mahabusu katika eneo hilo, wamelazimika kujenga seng’enge kama boma la mbuzi na watu wanaishi humo, hii ni aibu, nataka majibu ya Serikali ni kwa nini hali ibaki hivyo kwa muda mrefu,” alihoji Koka.
Katika swali lake la msingi ,mbunge huyo alitaka kujua kama Serikali haioni haja ya kulifanyia ukarabati Gereza la Mkuza lililojengwa mwaka 1995/96, likiwa na uwezo wa kuchukua mahabusu 45.
Kwa sasa gereza hilo linachukua mahabusu 150.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereila Silima alikanusha madai ya mbunge kuwa gereza hilo limesahaulika. Hata hivyo alisema tayari Serikali ilishaanza kulifanyia ukarabati gereza hilo. Alisema katika kipindi cha hivi karibuni, Serikali ilijenga mabweni mawili kwa ajili ya kuondoa kero kubwa iliyokuwepo katika Gereza la Mkuza na kuwa majengo hayo yako katika hatua za mwisho.

Wednesday, 24 April 2013
MREMBO ABAMBWA KWA WIZI CHUMA ULETE!
MREMBO mmoja, Rukia Omari mkazi wa Mbezi Beach jijini Dar amebambwa akidaiwa kuiba fedha kwa njia za miujiza eneo la
Bunju Mwanjenje kwenye duka la Wapemba.
Imeelezwa kuwa katika tukio hilo, Rukia alichukua fedha kimiujiza dukani na kutokomea, hali iliyosababisha wenye duka kutangaza dau la shilingi 500,000 kwa atakayewezesha kukamatwa kwake.
Arobaini zake zilipowadia, Rukia alikamatwa akiwa mafichoni, Boko Mtambani na kushushiwa kichapo na wananchi wenye hasira
wakimtaka amtaje aliyemtuma.
wakimtaka amtaje aliyemtuma.
Baada ya kupokea kichapo, mrembo huyo aliwataja baadhi ya watu akiwemo mganga mmoja anayetokea Sumbawanga (jina tunalo)
na kudai kuwa ndiye aliyekuwa akimpa dawa (chuma ulete).
na kudai kuwa ndiye aliyekuwa akimpa dawa (chuma ulete).
“Dawa hiyo huwa naiweka kwenye pesa zangu nyumbani ili ziongezeke na nyingine huwa natembea nayo kwa ajili ya kujipatia
pesa,” alisema mrembo huyo.
pesa,” alisema mrembo huyo.
Mrembo huyo alikiri kufanikiwa kuiba mamilioni ya shilingi kwa kutumia dawa hiyo na kuomba asamehewe. Rukia aliokolewa na
ndugu zake pamoja na wasamaria wema waliompeleka kwenye Kituo cha Polisi cha Wazo alikofunguliwa mashtaka ya wizi.
Tukio hilo ni la pili kwa Rukia kwani mara ya kwanza alikamatwa Tabata jijini Dar es Salaam miezi michache iliyopita kwa tuhuma
kama hizo lakini akaachiliwa baada ya kuomba msamaha.
Tukio hilo ni la pili kwa Rukia kwani mara ya kwanza alikamatwa Tabata jijini Dar es Salaam miezi michache iliyopita kwa tuhuma
kama hizo lakini akaachiliwa baada ya kuomba msamaha.
chanzo:.globalpublisher
Amchinja mama yake akimtuhumu mchawi
Watu wawili wameuawa katika matukio mawili tofauti mkoani Mbeya, likiwamo la kijana kumchinja mama yake kwa kutumia kisu kama kuku baada ya kumtuhumu kuwa ni mchawi aliyemloga mkwe wake.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Barakael Masaki, jana aliwaeleza waandishi wa habari kuwa tukio la kijana kumchinja mama yake mzazi limetokea juzi majira ya saa 1:00 jioni katika kijiji cha Chobwe wilayani Ileje.
Alimtaja mwanamke aliyetuhumiwa kuwa ni mchawi na kisha kuchinjwa na mwanae kuwa ni Anna Panja (60) mkazi wa kijiji cha Chobwe.
Akisimulia tukio hilo, Masaki aliema kijana huyo aitwaye Michael Panja akiwa na mwenzake ambaye bado hajafahamika, walimvamia mama huyo nyumbani kwake akiwa amelala na mumewe Basale Panja (76), wakamchukua mama huyo na kumchinja shingoni kwa kutumia kisu na kusababisha kifo chake papo hapo.
Alisema baada ya kutenda unyama huo, Michael na mwenzake walitoroka na kwenda kusikojulikana.

Waliofukiwa mgodini 12 sasa waokolewa wakiwa hai
Dar es Salaam. Watu wanne wamenusurika kufariki dunia baada ya udongo wenye mawe kuwafukia chini katika shimo zaidi ya saa 12 walipokuwa wakichimba dhahabu katika Kijiji cha Patamela wilayani Chunya.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Deodatus Kinawiro alithibitisha k wa njia ya simu jana juu ya tukio hilo na kwamba lilitokea Ijumaa iliyopita, ambapo uokoaji ulifanywa na Kampuni ya Shanta Gold Mining inayochimba dhahabu kilometa 10 kutoka eneo la tukio.
Kinawiro aliwataja walionusurika kuwa ni Antony Rwegasira(28), Pascal Claud(33) , John Gideon(47) na Noni Kwandu (40) wote wakazi wa wilayani humo.
“Ni kweli lango la kuingia shimoni liliporomoka, lakini gogo lilinasa kwenye mwamba na kusababisha mawe makubwa yabaki eneo hilo’’, alisema
Aliishukuru Kampuni ya Shanta kwa msaada iliyotoa kuokoa maisha ya watu hao na kwamba bila ya vifaa vya kampuni hiyo wangekuwa marehemu.
Tuesday, 23 April 2013
Mr. Nice asaka mke Kenya
MSANII mkongwe aliyepotea kwa miaka minne, Lucas Mkenda, ‘Mr Nice’, amefunguka kuwa amepanga kuoa mwanamke kutoka nchini Kenya.
Akizungumza wakati wa mahojiano na kituo cha runinga cha Citizen, Mr Nice alisema kuwa, mbali na kufanya muziki katika nchi hiyo pia amekwenda kwa ajili ya kutafuta mke wa kuoa.
“Mbali na kuja kikazi, lakini pia nimekuja kutafuta mke wa kuoa, najua atapatikana na nitawaambia, hayo ni mambo ya kumwachia Mungu,” alisema.
Mr. Nice aliongeza kuwa baada ya kusimama kwa muda mrefu kazi ya muziki, kwa sasa amesaini mkataba mnono na Kampuni ya Grandpa Records ya nchini humo.
Msanii huyo amewahi kutamba na mtindo wa ‘Takeu’, ambao ulibamba mashabiki wengi kutokana na nyimbo alizokuwa akiziimba.
chanzo:daima
Lema ailiza tena CCM
KWA mara nyingine tena Mahakama ya Rufaa nchini, imetupilia mbali maombi yaliyowasilishwa na walalamikaji, Musa Mkanga, Agnes Mollel na Hapiness Kivuyo ya kutaka kupitia upya hukumu iliyomrejesha Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA).
Walalamikaji hao ambao ni wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kupitia kwa mawakili wao, Alute Mughwai na Modest Akida, walidai kutoridhishwa na hukumu hiyo iliyotolewa Desemba 21 mwaka jana.
Walikuwa wakidai kuwa kulikuwa na mapungufu katika hukumu hiyo, hivyo walilitaka jopo la majaji waliohukumu kesi hiyo kukubali kubatilisha uamuzi wao ili rufaa ya kesi namba 47/2012 waliyokuwa wamefungua isikilizwe upya.
Wakili Mughwai aliitaka mahakama ifutilie mbali hukumu hiyo kwa madai kuwa ilipingana kwa kiasi kikubwa na hukumu iliyotolewa katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.
Akitoa mfano wa kesi zingine mbalimbali zilizowahi kupatikana na mazingira kama kesi ya Lema, Mughwai alijikita katika kifungu cha 66(a) na (b), na 4(ii), ambavyo majaji walimwambia amevichanganya vibaya badala ya kufungua kila dai moja peke yake.
Hata hivyo wakili huyo alidaiwa kuwa kuna vifungu alikuwa anavisema kwa mdomo wakati hakuviweka katika maandishi.
MSIKILIZE Kajala ndani ya Take one clouds
Lady Jaydee afunguka ya moyoni
MSANII mahiri anayeendelea kutesa katika anga la muziki, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ wakati akitarajiwa kuachia albamu yake ya sita, ameelezea yale yaliyo moyoni mwake.
Albamu hiyo aliyoipa jina la ‘Nothing But The Truth’ ameelezea kile ambacho kimejificha katika moyo wake.
Akizungumzia ujio wa albamu hiyo, ambayo itaingia sokoni Mei 31, mwaka huu, ikiwa imewashirikisha wasanii kama Prof. Jay, Yahya, Njiwa na bendi yake ya Machozi, alisema kuwa anaamini itawabamba mashabiki kutokana na namna alivyoeleza yale anayojisikia kutoka moyoni mwake.
Albamu hiyo ina nyimbo saba, ambazo ni ‘Joto Hasira’, ‘Historia’, ‘When You Cry’, ‘Msichoke’, ‘Tell Him’, ‘Nimekusamehe’ na uliobeba albamu, ‘Nothing But The Truth’.
Albamu za msanii huyo ni pamoja na ‘Machozi’ aliyoitoa mwaka 2000, ‘Binti’, ‘Moto’, ‘Shukrani’ na ‘The Best of Lady Jaydee’ iliyotoka mwaka 2012.

Lissu: Fujo zitakoma bungeni Spika akiacha upendeleo
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, amesema fujo zitaisha bungeni ikiwa Spika wa Bunge, Naibu na Wenyeviti watafuata na kusimamia kanuni za Bunge bila kupendelea upande wowote.
Lissu, ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani bungeni, aliyasema jijini Dar es Salaam jana wakati akihojiwa na kituo cha televisheni cha ITV.
Alisema fujo hazitaisha kama watu hawatafuata kanuni na Spika kusimamia na kuzingatia mamlaka yake bila ya upendeleo wowote.
“Tatizo kubwa Spika anafanya kazi bila kufuata kanuni za Bunge. Kuna mambo mengine anayatolea maamuzi bila kufuata kanuni za Bunge. Mfano suala letu la adhabu tuliyopewa wabunge watano wa Chadema ya kutohudhuria vikao vitano. Hakuna katika kanuni za Bunge. Spika alipaswa kupeleka majina yetu katika Kamati ya Maadili ili ichunguze na kupendekeza adhabu kisha ipeleke taarifa bungeni na Bunge ndilo litoe adhabu," alisema.

Watesaji wa Kibanda, Ulimboka kitendawili
WATEKAJI na watesaji wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Nchini, Dk. Stephen Ulimboka, na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda, wanaendelea kuwa kitendawili baada ya Jeshi la Polisi kudai linaendelea na uchunguzi.
Wakata jeshi hilo likishindwa kuwatia mbaroni watesaji wa wanataaluma hao, limetamba kukamilisha uchunguzi wake kuhusu kesi inayomkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare na Ludovick Joseph.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Isaya Mungulu, kwa waandishi wa habari jana, jalada hilo limepelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa hatua zaidi.
Licha ya matukio ya Ulimboka na Kibanda kutokea muda mrefu ikilinganishwa na lile la Lwakatare, Mungulu alishindwa kujibu maswali ya waandishi kuhusu suala ambalo linaonekana kupigwa danadana.
Dk. Ulimboka alitekwa na kuteswa vibaya kwa kuumizwa sehemu mbalimbali za mwili na kung’olewa meno, kucha kisha kutelekezwa katika Msitu wa Mabwepande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, usiku wa kuamkia Juni 26, 2012.
Katika tukio linalofanana na hilo, Kibanda naye alivamiwa wakati akiingia nyumbani kwake na kupigwa kwa nondo kichwani, kutobolewa jicho la kushoto, kung’olewa kucha, meno mawili na kukatwa kidole.
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na makao makuu limeunda timu za wataalamu kuchunguza matukio hayo lakini hadi leo zimekuwa zikipigwa danadana ya kuwakamata wahusika.

Monday, 22 April 2013
KUTOKA USWAHILINI HADI UGHAIBUNI !
Tunapozungumzia watanzania waliozaliwa na vipaji na kufanikiwa kuvipigania na kuviendeleza vipaji hivyo hadi kufikia kiwango cha kimataifa jina la Sensei Rumadha Fundi aka Romi
hatuwezi kulikwepa,mtanzania mwenye makazi yake nchini marekani,kabla ya kujikita kule marekani alikuwa moja ya wanafunzi wa karate pale Zanakaki,Dar chini ya mwalimu wake
Sensei Natambo Guru Kamara Bomani (RIP), baada ya hapo akaenda kwa mafunzo zaidi nchini Japan,Sweden na Denmark,
akachaguliwa kwenda nchini India kwa mafunzo ya kuwa mtaalamu wa Yoga,Vipaji hivi vya Karate na Yoga ,Sensei Rumadha Fundi anaiwakilisha Tanzania kuwa nchi ya wenye vipaji .Sensei Rumadha Fundi ni mwalimu wa karate na yoga
mwenye utalaamu na upeo wa hali ya juu sana,tena mwenye nidhamu.
Sensei Rumadha Fundi (Romi)( 3rd Dan black belt), akiwajibika katika semina ya karate Dojo ya Sugarland, Texas USA katika seminar ya walimu wa karate (ma-sensei) wiki iliyopita chini ya uongozi wake Sensei Ramon Veras (7th Dan), wa Traditional Okinawan Goju Ryu Karate-Do.Sensei Rumadha ni mmoja wa walimu wa Kitanzania wa karate ambao wanafanya vizuri katika fani hii ughaibuni, ni matumaini yetu wahusika katika sekta ya michezo hasa upande wa mapambano kama ngumi, kick boxing, judo nk wataangalia uwezekano wa kupata mchango wao ambao unaweza kusaidia katika kuboresha wanamichezo wetu kufikia kiwango cha kimataifa na kuliletea sifa taifa letu.
VIDEO: Fid Q akimzunguzia Bi Kidude
Kanye West is Spending LOTS of Money to Be a Good Dad
All those tabloid stories about Kim and Kanye being on the rocks are apparently far from the truth. Instead, TMZ is reporting that Yeezy is actually dropping major bank to be a good dad-to-be. Well, at least a present one.
The rapper has been spending most of his time over in Paris — working on his new album, performing, etc. — but he's been at every single one of Kim's doctor's appointments. That means he's taken a private jet from Paris to L.A. each time. This has allegedly cost Kanye something like $100,000.
Mr. West apparently even calls Kim's doctor's before the appointments to make sure he's been briefed on everything and that his schedule will allow him to be present.
Plus, Kim has also flown to Paris on a private jet to visit her man.
So, you see: No problems here that a private jet can't fix.
See more Kim Kardashian pics here:

Ubunge wa Godbless Lema majaribuni tena
Mahakama ya Rufani Tanzania leo inaanza kupitia maombi ya mapitio ya hukumu ya Mahakama ya Rufaa iliyomrejeshea ubunge mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema.
Mahakama hiyo inapitia maombi hayo ambayo yaliwasilishwa mahakamani hapo na makada watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliopinga ubunge wa Lema, na kufanikiwa kumvua ubunge kabla ya Mahakama ya Rufaa kumrejeshea wadhifa wake wakitaja sababu za kuomba hukumu hiyo ipitiwe upya.
Kwa mujibu wa hati za maombi hayo zilizowasilishwa katika mahakama hiyo na makada hao kupitia wakili wao, makada hao, ambao ni wapigakura wametaja sababu sita za kuomba hukumu hiyo iliyotolewa na jopo la majaji watatu ipitiwe upya.

Wabunge wamtega Kikwete
WABUNGE wamepanga kuisulubu Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kwa kukwamisha bajeti ya Wizara ya Maji kama haitakuwa na dhamira ya kupunguza au kuondoa tatizo la maji, Tanzania Daima limebaini.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika viunga vya Bunge mjini hapa, umebaini kuwa wabunge wamechoshwa na kauli na ahadi za serikali kukabili tatizo hilo wakati hakuna dhamira ya kweli ya kuliondoa.
Wabunge wa vyama tofauti wanaotoka mkoa au wilaya moja zenye shida ya maji, wameunganisha nguvu kutaka kukwamisha bajeti hiyo.
Wizara hiyo kupitia kwa Waziri wake, Profesa Jumanne Maghembe inatarajia kusoma mwelekeo wa bajeti yake leo na itajadiliwa kwa siku mbili.
Katika mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, iliyopitishwa wiki iliyopita, wabunge wengi akiwemo wa Same Mashariki, Anna Kilango (CCM) walichangia kwa hisia kali suala la maji.
Mbunge wa Nkasi, Ally Kesi (CCM) ambaye mwaka jana alipata upendeleo maalumu baada ya kutishia kwamba angewaleta wanawake wa jimbo lake bungeni, alisema maji ni kero namba moja kwa sasa nchini.
Mbali ya kujadili tatizo hilo kwa hisia kali bungeni, nje ya ukumbi wa Bunge mjadala wa maji umetawala.
Uchunguzi wetu umebaini kuwa hofu ya wabunge wa CCM ni kwamba endapo serikali haitatenga fedha za kutosha kukabili kero hiyo, wanaweza kupoteza nafasi zao mwaka 2015.
“Kila mwaka serikali inakuja na lugha nzuri kueleza namna ya kutatua kero hiyo, lakini mwisho wa mwaka wa bajeti hakuna kitu. Safari hii patachimbika,” alisema mbunge mmoja wa mikoa ya kusini.
Baadhi ya wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam waliliambia Tanzania Daima kuwa safari hii moto utawaka kwani serikali ilisema imetenga mabilioni ya fedha kwa ajili ya kukabiliana na kero hiyo jijini humo na kwamba lingekuwa historia.
Wabunge kadhaa waliozungumza na gazeti hili na kuomba majina yao yahifadhiwe kwa hofu ya kunyimwa nafasi ya kuchangia, walisema kwa nyakati tofauti kwamba wasipotengewa fedha kwa ajili ya miradi ya maji patachimbika.
Amuua baba yake kwa ushirikina
JESHI la Polisi mkoani Rukwa linamsaka Richard Jecap (30) mkazi wa kitongoji cha Matai A kwa tuhuma za kumuua baba yake kwa kumpiga mpini kichwani akimtuhumu kuwa ni mshirikina.
Tukio hilo lilitokea Aprili 18 saa 4.50 asubuhi wakati baba huyo akiwa amekaa nyumbani kwake akiota jua.
Tukio hilo lilitokea Aprili 18 saa 4.50 asubuhi wakati baba huyo akiwa amekaa nyumbani kwake akiota jua.
Alisema kuwa Aprili 16 mtoto wake wa pili mwenye umri wa miaka miwili alifariki na alidai kuwa baba yake ndiye aliyemloga kwani amekuwa akiloga watoto wake hao na siku ya mazishi aliahidi kumfanyia kitu kibaya baba yake huyo licha ya kuwa hakueleza ni kitu gani.
Saturday, 20 April 2013
Kajala ajutia kumdharau mama yake
MSANII maarufu wa filamu nchini, Kajala Masanja juzi alimwaga chozi kwa madai ya kujutia utovu wake wa nidhamu aliokuwa akimwonesha mama yake mzazi siku zilizopita.
Kajala ametoka kukumbana na kashikashi katika maisha yake hivi karibuni, baada ya kusota jela takriban mwaka mmoja kutokana na kesi ya kutakatisha fedha iliyomwandama yeye na mumewe ambaye yuko jela.
Akizungumza katika kipindi cha ‘Take One’ kinachorushwa kila Jumanne na Clouds Tv, Kajala alisema alipokuwa jela alimkumbuka mama yake kwa mambo aliyokuwa akimwambia na kuanza kujuta kutokana na mateso aliyokutana nayo huko.
“Mimi nilianza kumkumbuka sana mama yangu alivyokuwa akiniusia kutulia, ila mimi natoroka nyumbani nakwenda ninakotaka na kumuacha katika huzuni, ila nilipokaa jela niliona nini umuhimu wa mama, namuomba anisamehe sikujua nilitendalo,” alisema Kajala.
Aidha, Kajala alisema katika familia yao, mama yake alikuwa ni mkali kuzidi baba yake, ambaye kila kitu walichotaka kufanya aliwaruhusu, ikiwa ni pamoja na kwenda katika majumba ya muziki, lakini mama yao alikataa na kudai sasa anatambua umuhimu wake.
Aliwashukuru wote ambao walikuwa naye bega kwa bega hadi kufanikisha kutoka jela, hukushukrani za pekee akizimwaga kwa msanii mwenzake Wema Sepetu ambaye alimnusuru kufungwa jela miaka saba kwa kumlipia faini ya sh milioni 13.
chanzo:daima
Baba afungwa maisha jela kwa kumbaka mtoto wake
Sumbawanga. Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Mpanda, katika Mkoa wa Katavi, imemhukumu Abisai Joseph (40) wa Mtaa wa Kigamboni, kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wake.
Hukumu hiyo kesi hiyo iliyovutia watu wengi wa mji ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Chiganga Tengwa.Ilidaiwa kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Desemba 18 mwaka jana, akiwa nyumbani kwake.
Mwendesha Mashtaka, Ally Mbwijo, aliileza mahakama kuwa siku ya tukio, Abisai alimbaka mwanaye wa umri wa miaka sita.
Alidai kuwa mshtakiwa alifanya hivyo baada ya kumvizia mtoto huyo wakati alipotoka nje kwa lengo la kujisaidia haja ndogo
Aliiambia mahakama kuwa baada ya kumaliza kumfanyia kitendo hicho cha kinyama, mtoto huyo aliingia ndani huku akilia, jambo lililoshtuma mama yake na kumuuliza mumewe, kulikoni. Mwendesha mashtaka alidai kuwa katika majibu yake, mshtakiwa alidai kuwa alimkuta mtoto nje akibakwa na mjumbe wao wa nyumba kumi
Chadema wamtangazia vita Spika Makinda
Dodoma. Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amesema kuwa watakata rufaa katika Kamati ya Kanuni ya Bunge dhidi ya mwongozo wa Spika uliobariki adhabu ya kuwatimua kwa siku tano wabunge sita wa Chadema kwa kudharau mamlaka ya Spika.
Akitoa mwongozo wake jana, Spika Anne Makinda alibariki wabunge hao kutimuliwa akisema kuwa Kanuni za Bunge zilikiukwa.
Wabunge waliofukuzwa na Naibu Spika, Job Ndugai juzi ni pamoja na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia, Mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.
Juzi Mbowe aliomba mwongozo wa Spika kwa kutumia Kanuni ya 68 (7), akimtaka Spika aeleze naibu wake (Ndugai) alitumia kanuni gani ya Bunge, kuwasimamisha siku tano wabunge sita wa Chadema wasihudhurie vikao vya Bunge vinavyoendelea.
Mwongozo wa Makinda
Akitoa mwongozo huo jana, Spika Anne Makinda alisema kuwa kitendo kilichotokea hakiwezi kupuuzwa na wala kuvumiliwa na Bunge, pamoja na wananchi kwa kuwa ni utovu wa nidhamu ya Bunge na wananchi kwa jumla.

Alisema: “Kanuni ya 2(2) na 5(1), inampa mamlaka Spika ya kuleta amani bungeni.
Friday, 19 April 2013
Hakeem 5 - Nitunzie (Official Video)
Wanaotumia laini za simu zisizosajiliwa kutozwa Sh500,000 au kufungwa
Dar es Salaam. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kisheria mtu anayetumia simu isiyosajiliwa akikamatwa anaweza kutozwa faini ya Sh500,000 au kwenda jela miezi sita.
‘‘Kwa mujibu wa kifungu cha 131 cha sheria ya mawasiliano mteja au muuzaji wa namba ya simu ambayo haijasajiliwa atatozwa faini ya Sh500,000 au kifungo cha miezi mitatui’’ ilielezwa jana.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma alisema hayo alipokutana na wadau wa mawasiliano jijini hapa jana. Profesa Nkoma alisema namba za simu ni lazima zisajiliwe kwa mujibu wa sheria ya mawasiliano ya elekroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010.
Ufafanuzi wa TCRA umekuja baada ya kuwapo malalamiko ya watu wa kada mbalimbali kwamba mawasiliano yao ya simu yanaingiliwa na kuchapishwa katika vyombo vya habari.
Katika maelezo yake ya jana, Pofesa Nkoma alisema kwa mujibu wa kifungu cha 130 cha sheria ya EPOCA ya mwaka 2010, mtu ambaye atauza au kutoa namba za simu bila ya kusajiliwa atachukuliwa hatua za kisheria na adhabu yake ni faini ya Sh3 milioni na kifungo cha miezi 12
Bi. Kidude kama Tupac Shakur
MAISHA ya mwimbaji, Bi. Kidude, yamefikia ukomo Aprili 17, yakihusisha namba saba ambayo imewahi kufikisha ukomo wa msanii marehemu wa nchini Marekani wa kizazi cha sasa maarufu kama Tupac Omaru Shakur, aliyezaliwa Juni 16, 1971 na kufariki dunia Septemba 13, 1996.
Kifo cha mwanamama huyo kinafanana na Tupac kwa namba saba, kwa sababu matukio yaliyomtokea rapa huyo yalikuwa yakihusisha namba hiyo.
Kifo cha Tupac kilikuwa hivi; alipigwa risasi Septemba 7, miezi saba baada ya kuachia albamu yake ya ‘All Eyez On Me’, na alifariki dunia muda wa siku saba baada ya kupigwa risasi na alipigwa risasi saba na baada ya kifo chake ilitoka albamu yake iliyokuwa na jina la ‘The Don Killuminati’, ikimaanisha ‘Siku Saba za Nadharia’.
Hesabu ya miaka 25 ya 2pac aliyoishi kihesabu inahusishwa na namba saba (2+5=7) hata kifo chake kimahesabu kinaonesha alifariki dunia majira ya saa saba.
Namba hiyo inaonekana kwa Bi. Kidude kuanzia katika maisha yake binafsi ambapo alizaliwa Kijiji cha Mfagimarigo, Unguja katika familia ya watoto saba, amefariki dunia majira ya saa saba na maziko yake kufanyika majira ya saa saba. Pia aliolewa katika ndoa saba.
Maisha yake
Thursday, 18 April 2013
FARAJA KOTA, MUMEWE KAMA OBAMA NA MICHELLE
MREMBO aliyewahi kushika Taji la Miss Tanzania, Faraja Kota na mumewe Mheshimiwa Lazaro Nyarandu wamefananishwa na Rais wa Marekani, Barak Obama na mkewe Michelle Obama kutokana na muonekano wao.
Hivi karibuni mtandao wa 8020 fashion, ulitupia picha za Faraja na mumewe wakiwa wameongozana kwenye hafla ya uzinduzi wa mtandao wa www.shlendrect.co.tz ambapo wawili hao walionekana wakishikana mikono kama wafanyavyo Obama na mkewe
Kupitia mtandao huo, watu walitupia maoni na kusema kuwa wanandoa hao maarufu wanapaswa kuigwa na watu maarufu wote kwani wamewafananisha na Rais Obama na mkewe ambao wana heshima kubwa katika jamii
chanzo:globalpublishers.info
Mh.Peter Serukamba alipotumia neno F* Bungeni
Wafadhili waangusha chozi wanafunzi kukaa chini
MBUNGE wa Viti Maalumu, Susan Kiwanga (CHADEMA) na maofisa wa Benki ya NMB
Tawi la Kilombero, wamejikuta wakidondosha machozi baada ya kushuhudia wanafunzi
wakiwa wamekaa kwenye tope huku wakiendelea na masomo.
Tukio hilo lilitokea juzi katika shule za msingi Ntyangimbole na Kidete, zilizopo wilayani hapa wakati viongozi hao walipopeleka msaada wa madawati.
Pia viongozi hao walilazimika kuchangishana fedha papo hapo kwa ajili ya kununua mbao mbili za kuandikia walimu darasani.
Uamuzi huo ulifikiwa baada ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Ntyangimbole, Emmanuel Njavike, kusema kuwa mbali na watoto kukaa kwenye tope, hakuna vifaa vya kufundishia kama mbao za kuandikia, meza na vitabu, hivyo kuwalazimu walimu kufundisha kwa uzoefu.
Katika risala ya Shule ya Msingi Nyangimbole iliyosomwa na Mwalimu Asunta Mbuja, mbele ya ujumbe huo uliotoa madawati 38 kwa kila shule, walimu hao walisema ukosefu wa madarasa imara umetokana na serikali kutelekeza nguvu kazi za wananchi waliojitokeza kujenga vyumba viwili vya madarasa.
Wakijibu madai hayo kwa nyakati tofauti, Mbunge Susan aliahidi kufikisha kilio hicho bungeni kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na kulishawishi baraza la madiwani katika halmashauri hiyo kuangalia uwezekano wa upendeleo maalumu kuziwezesha shule za pembezoni kuwa na majengo imara ili wanafunzi wapate elimu bora.

TABIA YA MASHOGA (MASHOSTI)KUTEMBEA NA MWANAUME MMOJA KIMAPENZI NI AIBU KEMEA KEMEA!(WEMA NA PENNY)
WEMA NA PENNY
WEMA NA DIAMOND
PENNY NA DIAMOND
Tabia za wanawake wamjini zinatia kinyaa pale unapoona mtu na rafiki yake washare mwanume,
Hata kama rafiki yako kaachana na mpenzi wake sio sababu ya wewe kuwa mahusiano naye uko kunaitwa kujidhalilisha na kuoneka mbabaikaji fanyeni kazi jitumeni msiwe wavivu wa kufikili na kujituma
'Dawa za kuongeza nguvuza kiume sasa tishio Z'bar'
Waziri wa Afya Zanzibar, Juma Duni Haji, ameshangazwa na wimbi la uuzaji wa dawa za nguvu za kiume uliojitokeza katika maeneo ya misikiti visiwani humu.
Akifunga mjadala kuhusu ripoti ya Kamati ya Maendelo na Ustawi wa Jamii, Wanawake na Watoto ya mwaka 2012/2013 , Duni alisema waganga wamevamia maeneo ya misikiti na kuuza dawa za kienyeji zinazodaiwa kuongeza nguvu za kiume.
Duni alisema inashangaza kuna dawa zinazouzwa na za wanaume pekee lakini akasema ni jukumu la wananchi wenyewe kuwa makini kwa vile siyo kila daktari wa tiba asilia anaweza kutibu kila aina ya maradhi.
Hata hivyo, alisema kwa upande mwingine, vyombo vya habari vimekuwa vikichangia kuwaingiza wananchi katika matumizi ya dawa ambazo hazijathibitishwa ubora wake kutokana na kutangaza bila kupata ukweli wa dawa hizo.
Alisema baadhi ya dawa zinazouzwa huchangia matatizo ya wagonjwa kutokana
na kuzitumia bila maelekezo ya kitaalam, hivyo wanapozidiwa na kwenda
hospitali, ugonjwa huwa mkubwa na wengine kupoteza maisha.
Hata hivyo, Duni alisema ataendelea kusimamia ukweli kwa vile umri wake
unafikia ukingoni.
Alisema serikali imeshatunga Sheria ya Afya ya Jamii na Mazingira namba 11
ya mwaka 2012 ambayo itasaidia kuondoa matatizo ya matumizi mabaya ya tiba
asilia.
chanzo:nipashe
chanzo:nipashe
Wednesday, 17 April 2013
BURIANI "BI KIDUDE" TULIKUPENDA SANA ILA MUNGU ALIKUPENDA ZAIDI UPUMZIKE KWA AMANI
Justin Bieber May Soon Become the 'Make a Wish' Foundation's Greatest Wish-Granter
Justin Bieber's been getting a lot of criticism over all the topless selfies he's been posting to Instagram lately, but maybe the guy is just trying to keep his fans happy. He is a particularly skilled wish-granter, after
In 2012, WWE wrestler John Cena was honored by the organization for having granted 250 wishes. In his first two years working with the organization, Bieber granted 90 wishes, and has apparently outpaced other celebrities working with the organization.
For the full rundown on Bieber's impressive giving history, check out this article on The Inquisitr, which is the best press the poor kid has gotten since his 19th birthday

Subscribe to:
Posts (Atom)